Treni ya abiria iliacha reli na kuanguka kwenye stesheni nje ya mji wa Paris. Ajali hiyo imetokea katika mkesha wa siku kuu muhimu nchini Ufaransa. Mabehewa mawili yaliacha reli na kuyagonga magari.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, watu wasiopungua saba wamekufa na wengine kadhaa walijeruhiwa ,lakini amesema idadi ya watu wanaokufa kutokana na ajali hiyo inaendelea kubadilika.
Treni hiyo ilikuwa na abiria karibu mia nne, ilipoacha reli, umbali wa kilometa 20 kusini mwa mji wa Paris,alfajiri ya jana. Uchunguzi unafanywa ili kubainisha kilichoisababisha ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO