Monday, July 08, 2013

ARAB LEAGUE NI CHOMBO CHA WENYE FIKRA MBOVU

Spika wa Bunge la Syria amesema kuwa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ni chombo kinachotumiwa na viongozi wa Ghuba ya Uajemi kwa ajili ya kufikia malengo yao. Mohammad Jihad al-Laham ameongeza kuwa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inayojulikana kwa jina la Arab League ni wenzo wa viongozi wa Ghuba ya Uajemi wenye fikra finyu kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kisiasa. Spika wa Bunge la Syria ametahadharisha kuhusiana na njama za kugawanywa nchi za Mashariki ya Kati na kusema kwamba, nchi za eneo la Mashariki ya Kati zinakabiliwa na hatari ya kugawanya. Spika huyo wa Bunge la Syria amezikosoa vikali siasa za viongozi wa Ghuba ya Uajemi na njama zao za kuitumia Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kama wenzo wao wa kufikia malengo ya kisiasa. Amesema, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imesahau hata kadhia muhimu ya Palestina na dhulma wanayotendewa wananchi madhlumu wa Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema, inasikitisha kuona nchi hizo zinawaunga mkono magaidi wanaoendesha harakati zao nchini Syria na kupiga ngoma ya kutumiwa nguvu za kijeshi dhidi ya Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO