Habari kutoka Pakistan zinasema kuwa watu 17 wameuawa katika eneo la mpakani la Waziristan baada ya ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kuwashambulia kwa makombora usiku wa kuamkia leo. Ingawa jeshi la Marekani limesema kwamba waliouawa ni wanamgambo wa Taliban, lakini wananchi katika eneo hilo wanasema raia wa kawaida wakiwemo wanawake na watoto ndio waliouawa. Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif amesema uchunguzi utafanywa na ikibainika kwamba Marekani imewaua raia wasio na hatia kwenye hujuma hiyo Islamabad itaitaka Washington kuwalipa fidia waathirika. Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kutekeleza hujuma ya aina hiyo katika eneo hilo la kikabila la Waziristan tangu Nawaz Sharif ashike hatamu za uongozi nchini Pakistan mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO