Monday, July 08, 2013

CHAMA CHA BROTHERHOOD CHASEMA JESHI LIMEWAUA WAFUASI WAKE 34

Takriban Watu 34 wameuawa baada ya kuwepo Mapigano makali kati ya Vikosi vya kijeshi nchini Misri na Waandamanaji walio wafuasi wa Chama cha Muslim Brotherhood jijini Cairo. Vyanzo vya kitabibu nchini humo vimesema Watu 16 wameuawa, lakini Chama hicho kimedai kuwa Wafuasi wake 34 wamauawa katika mashambulizi ya Risasi. Jeshi limedai kuwa kundi la kigaidi lilikuwa likijaribu kushambulia eneo ambalo linaloripotiwa kuwa, aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Morsi anashikiliwa humo.
 Katika hatua nyingine, Chama cha Al- Nur hii leo kimetangaza kujiondoa kwenye mazungumzo juu ya kuundwa kwa Serikali mpya kwa kile walichodai kutokana na hali ya sasa na Mauaji dhidi ya Waandamanaji wanaotoa wito wa kumrejesha Morsi madarakani. Chama cha Al-Nur, kilichojinyakulia karibu Robo ya Kura za Bunge katika uchaguzi wa mwaka 2011 kiliunga mkono kuondolewa kwa Morsi Madarakani. Wafuasi wa Chama cha Muslim Brotherhood wamejikusanya kwa wingi katika maeneo mbalimbali jijini Cairo siku za karibuni, wakiapa kumtetea Morsi aliyepinduliwa na Jeshi baada ya maandamano makubwa yaliyoshinikiza kuondolewa Madarakani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO