Monday, July 08, 2013

MCHAKATO WA KUPATIKANA AMANI UTURUKI WAFIFIA

Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tyyip Erdogan amedhihirisha ahadi yake ya kushiriki katika mchakato wa maridhiano na Watu jamii ya kikurdi takriban Milioni 15, hata hivyo matukio ya hivi karibuni yanadhihirisha kuwa Mchakato wa kuelekea kupatikana kwa amani hautafanikiwa. Tangu kuibuka kwa Maandamano mjini instambul tarehe 31 mwezi May, ikifuatiwa na miji mingine nchini Uturuki,kisha Mchakato wa kuweka silaha chini uliotangazwa na Chama cha Kikurdi PKK, wa tarehe 21 mwezi Machi kuwa kazi bure. Siku ya jumanne, juma lililopita Erdogan alitoa Wito kwa Watu na Subira na kutangaza kuwa yuko tayari kufanya michakato ya kupatikana kwa amani nchini humo akiapa kuwa hakuna atakayemzuia kutekeleza hilo.
 Watu wa Jamii ya Kikurdi wameeleza kuchoshwa na ahadi walizodai hewa na kushindwa kwa Erdogan katika kutekeleza matakwa yao. Wakurdi wamekuwa wakidai katiba ya Uturuki kuwatambua na kuruhusiwa kufundisha lugha ya kikurdi kwenye shule za Serikali. Waziri wa mambo ya ndani ya Uturuki Muammer Guler amesema kuwa hakuna maendeleo yoyote ya kufikiwa kwa amani kati ya pande mbili mpaka pale wapiganaji wa PKK watakapoondoka kabisa. Guler amesema kuwa Sharti lililowekwa kwa ajili ya kufanyika kwa mazungumzo halijatekelezwa kwa kuwa wapiganaji wa PKK bado wako nchini Uturuki ingawa walitangaza kuacha mapigano.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO