Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita nchini Bangladesh imemuhukumu kifungo cha miaka 90 jela kiongizi wa kiislamu Ghulam Azam baada ya kumkuta na hatia ya makosa yote matano yaliyokuwa yakimkabili kuhusiana na vita vya harakati za ukombozi mwaka 1971 toka kwa nchi ya Pakistan. Ghulam Azam mwenye umri wa miaka 90 hivi sasa anatuhumiwa kushiriki kuunda vikundi vya uasi wakati wa vita hivyo ambapo vilihusika kupanga, kutekeleza mauaji na kushiriki vetndo vya ubakaji dhidi ya raia. Wafuasi wa chama cha kiislamu cha Jamaat --Islam kilichokuwa kinaongozwa na Ghulam toka mwaka 1969 hadi 2000 wamekabiliana na polisi nje ya mahakama hiyo kabla na baada ya hukumu kusomwa.
Mahakama hiyo imemkuta na hatia ya makosa yote matano ikiwemo uchochezi, kupanga njama kutekeleza mauaji, kushindwa kuzuia mauaji, ubakaji na uhalifu dhidi ya binadamu. Ghulam mwenyewe amekanusha kuhusika na machafuko ya nchini mwake wakati wa harakati za kupigania uhuru wake toka kwa taifa la Pakistan na kudai kuwa kesi yake ni yakisiasa. Wafuasi wa Ghulam wameapa kufanya maandamano kupinga hukumu hiyo ambayo nao wanadai ilichochewa kisiasa. Awali mwendesha mashtaka wa Serikali aliiomba mahakama kumuhukumu kunyongwa Ghulam kutokana na makosa ambao aliyatekeleza wakati akiwa kiongozi wa chama.
Zaidi ya watu laki tatu wanaelezwa kupoteza maisha nchini Bangladesh wakati wa vita vya uhuru, huku Ghulam akitajwa kuhusika kwa sehemu kubwa kutekeleza mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO