Sunday, July 14, 2013

MJUE MAMA WA WAUMINI KHADIYJAH (RA)

NASABA YAKE 
Jina lake ni Khadija binti Khuwaylid bin Asad bin Abdul Uzza Qusay bin Kilab anayetokana na kabila la Kikureshi aliyezaliwa katika mwaka wa 68 kabla ya Hijra yaani mwaka 556 baada ya Nabii Issa (Alayhis Salaam). Wazee wake walimlea kwa heshima na adabu ya hali ya juu na alikuwa akijulikana kwa jina la ‘Aliyetakasika’ hata kabla ya kuja kwa Uislamu.

ANAOLEWA NA ATIYQ BIN AIDH
Imepokelewa kuwa siku moja vijana wa kabila la Kikureshi walipokuwa wamekaa karibu na Al Kaaba wakizungumza, aliinuka mmoja wao anayeitwa Al Harith akasema:
“Enyi ndugu zangu nimetia nia ya kuowa”.
Mmojawao akamwambia:
“Uamuzi mzuri huo, kwani tokea alipofariki mama yako na baada ya baba yako kuowa mke mwingine umekuwa unaishi peke yako”.
Mwengine akasema:
“Umefanya vizuri kuamua kuoa, kwani kila mwanamke anatamani kuolewa na mtu kama wewe, maana baba yako ni katika watu wanaoheshimika katika kabila la Kikureshi, na wewe unamiliki mali nyingi sana, sidhani kama yupo mwanamke atakayekukataa”.
Al Harith Akawatizama wenzake kwa muda, kisha akasema:
“Nyinyi mnadhania hivyo kwa sababu ni rafiki zangu, lakini mnakosea”.
“Tunakosea vipi?  Hebu tufahamishe”.
Akawaambia:
“Nilitaka kumuowa Khadija, lakini baba yake alinikatalia kwa sababu eti anasema kuwa kabila langu ni duni kuliko kabila lake”.
Wenzake wakasema:
“Bila shaka hiyo, kwani Khadija ni binti wa Khuwaylid bin Asad naye ni mtu mtukufu miongoni mwa mabwana wa kabila la Kikureshi mwenye kumiliki mali nyingi sana na nyumba kubwa ambayo daima inapokea wageni mbali mbali wanaokuja Makka”.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO