Wajumbe kutoka Korea Kaskazini na Korea kusini wameanza mazungumzo leo ya kukifungua tena kiwanda cha pamoja cha Keosong ambacho ndio ishara pekee ya ushirikiano wa nchi hizo mbili hasimu.Eneo hilo la viwanda lilifungwa mwezi April kutokana na kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo baada ya Korea Kusini kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Marekani na kuwekewa vikwazo Korea Kaskazini kwa sababu ya majaribio yake ya makombora ya kinyuklia.Nchi hiyo iliamuru kufungwa kwa eneo hilo la viwanda na kuwaondoa wafanyakazi wake 53,000.Wizara ya ushirikiano ya Korea Kusini imesema pande hizo mbili zimeanza mazungumzo katika kijiji cha suluhu cha Panmunjom na wamesikilizana kujadili kuchukuliwa kwa bidhaa ambazo mameneja kutoka Kusini waliziacha katika eneo hilo la viwandani pamoja na kukagua viwanda hivyo.Pia watajadili kuanza tena kwa kazi huko Keosong. Mazungumzo hayo yanawadia baada ya tofauti za ikitifaki mwezi uliopita kuwamisha mazungumzo ambayo yangelikuwa ya kwanza ya ngazi ya juu kuwahi kufanyika baada ya miaka mingi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO