Tanzania imemkamata raia wa Uingereza anayeshukiwa kuhusika katika vitendo vya kigaidi nchini Uingereza. Polisi wa eneo la kusini mwa Mbeya wamesema wamemkamata Iqbal Ahsan Ali akiwa na hati za usafiri za Uingereza na Tanzania ambalo ni kosa la jinai nchini Tanzania kutokana na kupigwa marufuku kwa uraia wa nchi mbili nchini humo.
Mkurugenzi wa upelelezi wa jinai Robert Manumba amesema wamekuwa wakiwasiliana na wenzao wa Uingereza na wamethibitisha kuwa mshukiwa huyo anatakikana nchini mwake kwa kushiriki katika vitendo vya kigaidi.Watu kadhaa wamekamatwa nchini Tanzania kwa mashitaka ya ugaidi tangu mashambulio ya mabomu kuwaua watu wanane mwezi Mei na Juni nchini humo.Maafisa wa usalama nchini humo wana wasiwasi na ongezeko la harakati za makundi ya Kiislamu yenye itikadi kali yaliyo na mafungamano na waasi wa Al Shabab.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO