Saturday, July 06, 2013

MAJESHI YA SYRIA YAKARIBIA KUUDHIBITI MJI WA HOMS

Mwanaharakati mmoja na shirika la habari la taifa nchini Syria wamesema wanajeshi wa utawala wa Rais Bashar al Assad wanaelekea katika sehemu kadhaa za mji unaodhibitiwa na waasi wa Homs.Tarik Badrakhan mwanaharakati aliye katika mji huo  leo amesema kuwa majeshi hayo yamedhibiti majengo katika eneo la Khaldiyeh hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa serikali kuingia miji iliyo karibu na Homs katika kipindi cha mwaka mmoja.Shirika la habari la taifa nchini humo limeripoti kuwa wanajeshi hao wanakaribia mji huo na wamewaua waasi katika eneo hilo.Badrakahn amesema wanajeshi hao walianza operesheni hiyo jana usiku na kufikia leo walikuwa wanaendelea kulivamia eneo hilo kwa makombora  ikiwa ni operesheni kubwa kuwahi kufanywa na wanajeshi hao wa Assad kujaribu kuukombowa mji huo unaodhibitiwa na waasi.Homs ni mji muhimu ukiwa kati ya mji mkuu Damascus na mwambao wa Syria ambayo ni ngome kuu ya utawala wa Assad.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO