Serikali ya Marekani imesema itaendelea kuwalisha kwa nguvu Mwezi wa Ramadhani wafungwa waliosusia kula katika jela ya Guantanamo inayosimamiwa na Jeshi la Marekani.
Wizara ya Sheria ya Marekani imedai kuwa wafungwa watalishwa usiku tu lakini Baraza la Waislamu Marekani (CAIR) limewataka wakuu wa Jela ya Guantanamo kuacha kuwalisha kwa nguvu wafungwa baada ya Jumatatu.
Zaidi ya wafungwa 100 waliosalia katika jela hiyo ya kutisha walianza mgomo wa kutokula chakula tangu mwezi Februari mwaka huu wakilalamikia hali mbaya ya jela hiyo, kuporwa vitu vyao zikiwemo barua, kudhalilishwa na kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu, hususan nakala za Qur’ani Tukufu. Mkenya pekee anayeshikiliwa Guantanamo, Abdulmalik Mohammad, amejiunga na wafungwa wenzake ambao wamesusia chakula kama njia ya kulalamikia kuendelea kushikiliwa pasina kufunguliwa mashtaka.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO