Saturday, January 12, 2013

100 WAUWAWA KATIKA MRIPUKO PAKISTAN


Zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa nchini Pakistan, kufuatia mfululizo wa mashambulizi yaliyowalenga askari wa usalama na raia wa nchi hiyo. Jana Alihamisi watu wasiopungua 90 waliuawa katika milipuko mitatu ya mabomu iliyotokea kwenye mji wa Quetta, makao makuu ya mkoa wa Balochistan. Mlipuko mwingine umetokea katika mji wa Mingora mkoani Swat na kupelekea watu 21 kupoteza maisha yao na wengine 60 kujeruhiwa.
Maelfu ya Wapakistan wamekuwa wakiuawa katika milipuko na mashambulizi tangu mwaka 2001, baada ya nchi hiyo kujiunga katika ushirika na Marekani kwa madai ya kupambana na vita dhidi ya ugaidi. Hii ni katika hali ambayo wimbi la mashambulio ya mauaji limekuwa likiwalenga Waislamu wa Kishia katika miaka ya hivi karibuni nchini Pakistan.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO