Tuesday, January 15, 2013

ALGERIA YAIRUHUSU UFARANSA KUTUMIA ANGA YAKE

Ufaransa imesema kuwa Algeria imeziruhusu ndege zake za kivita kutumia anga yake kuendeshea mashambulizi dhidi ya eneo la kaskazini mwa Mali. Laurent Fabius Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa amesema kuwa Algeria imeziruhusu ndege za nchi hiyo kutumia anga yake kuendeshea oparesheni dhidi ya wanamgambo wa kaskazini mwa Mali. Tangazo hilo limetolewa baada ya ndege za kivita za Ufaransa kuzishambulia ngome za waasi karibu na mji wa Gao huko kaskazini mwa Mali. Ufaransa ilianzisha oparesheni zake za kijeshi huko Mali Ijumaa iliyopita katika kile ilichokitaja kuwa ni katika kuzuia kusonga mbele waasi wanaodhibiti eneo la kaskazini mwa Mali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO