Thursday, July 04, 2013

KENYA YASUSIA SHEREHE ZA UHURU WA MAREKANI

Katika kile kinachoonekana ni kuendelea kuzorota uhusiano wa Nairobi na Washington, maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Kenya wamesusia sherehe za uhuru wa Marekani zilizofanyika jana usiku katika ubalozi wa Marekani mjini Nairobi.
Katika hafla hiyo ambayo maafisa wote wa ngazi za juu serikalini walialikwa, rais na naibu wake hawakuhudhuria, aidha hakuna waziri au katibu mkuu wa wizara aliyehudhuria hafla hiyo. Sherehe hizo zimekuja siku mbili tu baada ya Rais Obama kukamilisha safari yake ya kuzitembelea nchi za Afrika pasina kuitembelea Kenya kama ilivyotarajiwa. Afisa pekee wa serikali ya Jubilee aliyehudhuria sherehe hizo ni Spika wa Senate Ekwe Ethuro na maafisa wa ngazi za chini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.
Hivi karibuni Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake haibabaishwi na mitazamo ya nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikimpiga vita. Rais Kenyatta alisema mitazamo ya nchi za Magharibi haitaizuia serikali ya Jubilee kuwahudumia Wakenya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO