Rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki, amesema mtangulizi wake Nelson Mandela, huenda akatoka hospitali na kuendelea na matibabu nyumbani. Mbeki aliyasema hayo wakati akizungumza katika hafla moja ya chama cha Afriacan national Congress-ANC, mwishoni mwa juma.
Mandela amelazwa hospitali kwa wiki tano sasa kutokana na maambukizi ya mapafu, hali iliosababisha kumiminika kwa risala za kumuombea nafuu kutoka ndani ya Afrika kusini na kimataifa. Marafiki waliomtembelea wamesema Mandela bado anapumua kwa msaada wa mashine. Shujaa huyo wa vita dhidi ya sera ya ubaguzi wa rangi, alitumikia kifungo cha miaka 27 gerezani, kabla ya kuwa Rais wa kwanza wa Afrika kusini ya Kidemokrasia 1994. Thabo Mbeki aliyekuwa makamu wake wa Rais, alishika wadhifa huo wa kuiongoza Afrika kusini pale Mandela alipostaafu 1999.Alhamisi wiki hii Mandela atatimia umri wa miaka 95.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO