Monday, July 15, 2013

URUSI YASUBIRI OMBI LA SNOWDEN

Maafisa wa Urusi wamesema wanasubiri  ombi la hifadhi ya kisiasa kutoka kwa wakala wa zamani wa Shirika la ujasusi la Marekani CIA Edward Snowden, ikiwa ni siku tatu baada ya kusema ameamua kuomba hifadhi nchini Urusi.Idara ya uhamiaji ya Urusi imesema haikupokea ombi lolote hadi sasa na haiwezi kutoa taarifa zaidi. Duru moja ambayo haikutaka kutajwa jina, ilisema Snowden aliyefichua siri kwamba Marekani imekuwa ikichunguza na kunasa taarifa za washirika wake wa Ulaya, yungali katika  uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow, akiwa chini ya Ulinzi.
Mtumishi huyo wa zamani wa CIA aliyewasili  Moscow kutoka Hongkong, alikutana na wanaharakati wa haki za binaadamu  ndani ya uwanja huo wa ndege siku ya Ijumaa iliopita na  Mwanasheria mmoja maarufu Anatoly Kucherena akasema kwamba Snowden amesaini ombi la hifadhi ya ukimbizi. Marekani imekuwa ikidai ikabidhiwe  mtu huyo , takwa ambalo limekataliwa na  Rais wa Urusi Vladimir Putin.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO