Thursday, July 18, 2013

UJERUMANI YAPINGA KUUFAHAMU MPANGO WA KIJASUSI WA MAREKANI

Serikali ya Ujerumani leo imekanusha ripoti inayodai kuwa jeshi lake lilifahamu kwa miaka mingi kuhusu mpango wa ufuatiliaji wa Marekani, PRISM, uliofichuliwa na Edward Snowden, mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA. Shirika la ujasusi wa kigeni la Ujerumani, BND, limesema kuwa mpango mwingine wenye jina kama hilo ulikuwepo kwa ajili ya vikosi vya jumuiya ya kujihami ya NATO nchini Afghanistan kubadilishana habari za kijasusi. Msemaji wa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ambaye anashiriki katika uchaguzi wa Septemba 22, amesema hana sababu ya kutilia shaka taarifa ya shirika la BND. Suala hilo ni nyeti kwa Merkel, ambaye alisema wiki iliyopita kuwa alifahamu tu kuhusu upeo wa suala hilo la Shirika la Ujasusi la Marekani kupitia vyombo vya habari. Wajerumani wengi wana hasira kuwa ujumbe wao wa barua pepe, mawasiliano ya simu, na data nyingine zimenaswa na kuhifadhiwa katika mpango huo wa shirika la ujasusi la Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO