Monday, July 01, 2013

UMOJA WA MATAIFA WAKANUSHA KUWEPO USHIRIKIANO KATI YA IRAN NA KOREA

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa na haki Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika maelezo yake kuwa hakuna ushirikiano wowote wa kimakombora kati yake na na Korea Kaskazini. Ripoti ya kila mwaka ya jopo la kamati ya vikwazo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Iran inaeleza kuwa, hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuweko ushirikiano wa kiufundi kati ya Korea Kaskazini na Iran katika kuunda makombora ya masafa marefu. Tarehe 12 Disemba mwaka jana Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mojam, na muda mfupi baadaye Shirika la Habari la Japan Kyodo likanukuu duru moja ya kidiplomasia ya Magharibi ikidai kuwa, mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, Iran ilituma huko Korea Kaskazini, timu ya watu kadhaa  kutoka Wizara ya Ulinzi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa makombora ya nyuklia kati ya nchi mbili hizo. Hata hivyo madai hayo yalikanushwa tarehe 24 Disemba mwaka jana na Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi, Waziri wa Ulinzi wa Iran ambaye aliyataja madai hayo kuwa maneno matupu na kwamba Tehran haijamtuma mtu yeyote huko Pyongyang kwa ajili ya ushirikiano wa makombora.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO