Nchini Kenya Muungano wa Walimu wa shule za Sekondarina Vyuo KUPPET umetangaza kusitisha mgomo kwa muda ili kuruhusu mazungumzo na serikali.
Maafisa wa Kuppet wamewataka wanachama wao warejee darasani siku ya Jumatano ili muungano huo ufanye mazungumzo na serikali kama mahakama ilivyo amuru. Hatahivyo CHAMA cha Kitaifa cha Walimu (KNUT) kinasisitiza kuwa mgomo unaendelea.
Katibu Mkuu wa Kuppet Akelo Misori amesema Bodi ya Magavana cha chama hicho wamekutana leo Jumanne na kuamua kusitisha mgomo.
Mgomo wa walimu Kenya ulianza Juni 25, 2013 ambapo ilitazamiwa utaendelea hadi wakati ule serikali itakapowalipa walimu nyongeza ya marupurupu ambayo yaliafikiwa 1997, miaka 16 iliyopita.
Mahakama Kuu nchini Kenya Jumatatu iliwaamuru walimu wote wanaogoma warejee kazini Jumanne na kumtaka Waziri wa Leba Kazungu Kambi aunde kamati ya kushauriana na vyama vya walimu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO