Wednesday, July 03, 2013

MPALESTINA MMOJA AULIWA SHAHIDI NA MAJESHI YA ISRAEL

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamemuua shahidi kijana mmoja wa Kipalestina katika mapambano yaliyojiri karibu na mji wa al-Khalil (Hebron) katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi.
Imearifiwa kuwa, Moataz Sharawna aliyekuwa na umri wa miaka 19 ameuawa shahidi baada ya kukanyagwa na gari la deraya la jeshi la Israel katika kijiji cha Dura.
Tukio hilo limejiri baada ya mapambano ya usiku kucha baina ya wanamapambano wa Kipalestina na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.
Duru za Palestina zinasema mwaka huu wa 2013 wapalestina wasiopungua 16 wameuawa shahidi na wanajeshi wa Israel huku Wapalestina wengine 1,790 wakiwemo wanawake na watoto wadogo wakitekwa nyara katika kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO