Monday, July 15, 2013

WANASHERIA WA KIMATAIFA WAPINGA VIKWAZO DHIDI YA IRAN

Jopo la wataalamu wa sheria wa kimataifa limesisitiza kuwa, vikwazo vya upande mmoja vilivyowekwa na Marekani na nchi za Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si vya kisheria. Jopo hilo la wanasheria wa kimataifa limeeleza hayo kwenye kongamano lao lililofanyika hivi karibuni nchini Uholanzi na kusisitiza kwamba miradi ya nyuklia ya Iran ni ya amani, hivyo hakuna sababu kwa nchi hizo za Magharibi kutekeleza vikwazo hivyo. Jaji Abdul G. Koroma, jaji wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya The Hague amesema kuwa, vikwazo hivyo vya upande mmoja ni vya kidhuluma, kwani Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA umethibitisha mara kadhaa kwamba, miradi ya nyuklia ya Iran inafanyika kwa malengo ya amani. Huku akisisitiza kuwa, kisheria hakuna nchi au taasisi yoyote duniani iliyo na haki ya kuweka vikwazo vya upande mmoja, Jaji Abdul G. Koroma ameongeza kuwa, vikwazo vitakavyowekwa dhidi ya nchi yoyote kwa malengo ya kuiadhibu kidhulma, havina uhalali wa kisheria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO