Monday, July 15, 2013

CHAMA CHA UDUGU WA KIISLAM CHATISHIA KUUNDA JESHI

Kiongozi mkuu wa Harakati ya Ikhwanul Muslimiin nchini Misri amelitahadharisha Baraza Kuu la Vikosi vya Jeshi na vyama vya kisiasa vinavyompinga Muhammad Morsi  nchini humo kwamba, harakati hiyo  itaunda jeshi la ukombozi wa Misri kwa shabaha ya kuirejesha tena madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi nchini humo. Muhammad Badie amesisitiza kuwa, wananchi wa Misri wanaomuunga mkono Muhammad Morsi rais aliyeondolewa madarakani nchini humo wana haki ya kufanya maandamano kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali yake. Ameongeza kuwa, maandamano na machafuko yataendelea kushuhudiwa nchini Misri hadi pale utawala wa kisheria utakaporejeshwa nchini humo. Kiongozi huyo mkuu wa Ikhwaanul Muslimiin amesema kuwa, hivi sasa njia pekee ya kurejeshwa amani na utulivu nchini humo ni kuundwa jeshi la ukombozi wa Misri litakalowashirikisha baadhi ya wanajeshi walioko kwenye jeshi la nchi hiyo. Kiongozi huyo wa Ikhwanul Muslimiin amefichua kwamba, jeshi linapanga njama za kumuwekea Muhammad Morsi sumu kwenye chakula, ili kumdhuru kiakili.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO