Sunday, July 07, 2013

WAPINZANIA WA SYRIA WAPATA RAIS MPYA

Kundi  kuu  la  upinzani nchini Syria  la  Muungano  wa  Kitaifa  limemteua Ahmed Aasi al-Jarba , mfungwa wa kisiasa wa zamani kama rais mpya wa kundi  hilo.  Muungano huo umekuwa bila ya kiongozi tangu mwezi machi baada ya kujiondoa kwa Moaz al-Khatib.
Wanachama 115 wa muungano huo wanaoishi uhamishoni na ndani ya Syria walikutana kwa siku mbili mjini Istanbul Uturuki kumchagua kiongozi wao. Tayari Marekani imesema iko tayari kufanya kazi na Al Jarba.
Muungano huo uliundwa kwa mara ya kwanza nchini Qatar mwezi Novemba mwaka jana ukiwa na nia ya kuunganisha wapinzani wanaopigana kumuondoa madarakani rais wa Syria Bashar al-Assad.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 93,000 wameuwawa tangu kuanza kwa mapigano zaidi ya miaka miwili iliopita nchini humo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO