Thursday, July 11, 2013

WASHUKIWA WA BOKO HARAM WAFUNGWA MAISHA

Wanachama wanne wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mashambulio ya bomu yaliyosababisha vifo vya watu kumi na tisa. Wanne hao walipatikana na hatia ya kupanga na kutekeleza mashambulio ya mabomu katika ofisi za tume ya uchaguzi na kanisa moja mwaka uliopita.
Hukumu hiyo ndiyo kali zaidi kuwahi kutolelwa kwa mwanachama au mshukiwa yeyote wa kundi hilo la Boko Haram. Kundi hilo limehusika na mashambulio kadhaa ambayo yamesababisha maafa mengi katika maeneo ya Kaskkazini na Kati nchini Nigeria. Katika miaka ya hivi karibuni kundi hilo limekuwa likiwalenga raia wa kawaida na zaidi ya watu elfu mbili wameuawa tangu kundi hilo la Boko Haram kuanzisha uasi mwaka wa 2009, katika juhudi zake za kutaka kuundwa kwa taifa jipya la Kiislamu katika eneo lililo na idadi kubwa ya Waislamu Kaskazini mwa Nigeria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO