Saturday, July 13, 2013

WATUHUMIWA UGAIDI WAPANDISHWA KIZIMBANI KENYA

Mahakama ya Kenya imewafungulia mashtaka raia watatu wa kigeni kwa tuhuma za kufanya  ugaidi nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, watuhumiwa hao ambao wawili ni Wafaransa na mmoja Mbelgiji, walipandishwa kizimbani mjini Malindi, kwa tuhuma za kuingia nchini humo kinyume cha sheria. Taarifa zinasema kuwa, raia wawili wa Kenya pia siku ya Jumanne walitiwa mbaroni mjini Malindi, kwa tuhuma za kuwapa hifadhi kinyume cha sheria watuhumiwa hao. Taarifa zinasema kuwa, raia hao wa kigeni waliingia nchini Kenya kwa mara ya kwanza mwezi Aprili mwaka 2011 kwa viza ya mwezi mmoja, lakini baadaye walielekea nchini Somalia na kujiunga na kundi la al Shabab. Njiru Mwaniki  Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi nchini Kenya amesema kuwa, raia hao wa kigeni walitiwa mbaroni kutokana na mashirikiano na vyombo vya upelelezi nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO