Vyombo vya usalama vya Uholanzi vimemtia mbaroni mtu mmoja anayeshukiwa kwa kufanya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Msemaji wa Mahakama ya Uholanzi amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni siku ya Jumanne iliyopita nchini humo. Mahakama hiyo ilikataa kutaja utambulisho na wasifa wa mtuhumiwa huyo na kusisitiza kuwa, mtuhumiwa huyo aliomba hifadhi ya ukimbizi nchini humo mwaka 2011 na serikali ya Uholanzi ilikataa kumpa hifadhi hiyo kwa vile anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji kwenye shule moja mjini Kigali. Kwa mujibu wa sheria za Uholanzi, Mahakama za nchi hiyo zinapewa ruhusa ya kuwafuatilia na hatimaye kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa mauaji ya halaiki yaliyofanyika katika sehemu yoyote duniani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kwa akali Watutsi elfu mbili waliuawa kwa halaiki kwenye shule za mjini Kigali, vitendo vilivyofanywa na Wahutu wenye misimamo mikali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO