Friday, July 11, 2014

MASHAMBULIZI YA WAISRAEL KATIKA MSIKITI WA AL-AQSA


Wakati waislamu wote duniani waiwa katika mfungo wa Ramadhani, Wapalestina na maeneo mengine yenye waislamu hayana furaha. Tunashuhudia kwa siku ya pili sasa mauaji ya wanawake na watoto yakiedelea huko Gaza nchini Palestina. Hii ni moja ya video zilizosambaa mitandaoni ikionesha mashambulizi katika msikiti wa Al-Aqsa, miongoni mwa maeneo matukufu kwa waislamu. Jeshi la Israel ndo linatekeleza mashambulizi hayo bila huruma wala aibu yoyote ile huku taasisi za umoja wa mataifa na tasisi za haki za binaadamu zikikaa kimya kabisa. Pia vyombo vya habari tunavyovijua vya kimataifa vimekuwa washabiki wa upande mmoja wa habari, vikionesha kama vile israel imekuwa ikionewa wakati huohuo havioneshi ni jinsi gani wapalestina wakiuwawa hasa wale wasiokuwa na hatia kabisa kwani mashambulizi yamekuwa yanafanyika katika makazi ya watu na sio katika maeneo ya kivita. Mungu Awafanyie wepesi watu wa Palestina na audhalilishe utawala haramu wa kizayuni. Ameen!!  

Thursday, July 03, 2014

WANASAYANSI WAGUNDUA UCHAPISHAJI WA MISHIPA YA DAMU

Ogezeko la maendeleo ya kiteknolojia yamepelekea watu kufikiri njia mbadala za kurahisisha maisha zaidi. Katika swala la afya, tunashuhudia ugunduzi mkubwa wa kitabubu ambapo wanasayansi kutoka maeneo mbalimbali duniani wantumia muda wao mwingi katika utafiti. Mpaka leo bado kuna uhaba wa viungo vya binaadamu ambapo watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na uhaba huu. Njia inayotumika mpaka sasa ni ya kupewa viungo mfano wa figo kutoka kwa mtu mwingine. Miaka ya karibuni, watu walizindua mashine za uchapishaji wa vitu halisi yaani "3D printing". Sasa teknolojia hiyo inaunganishwa na afya kwa ajili ya kuchapisha viungo vya mwili "BioPrinter". Inashangaza lakini ni wazo zuri, fikiria mfano unaenda hospitali na unahitajika ufanyiwe upasuaji wa figo, bila kusita wala kutafuta mtu wa kukupa figo yake, basi inaenda kuchukuliwa kutoka kwenye maabara tu. Kwa sasa watafiti kutoka vyuo vya Sydney, Harvard, Stanford na MIT wamefanikiwa kugundua uchapishaji wa mishipa ya damu hasa katika mapafu. Wametumia utafiti wao na njia mbali mbali za kitabibu hatimae wamefanikiwa kuchapisha mfumo wa mishipa midogo sana ya damu ndani ya mapafu. 

Chanzo: Engadget

Tuesday, July 01, 2014

CHINA KUJENGA JENGO LA 1KM KWA UREFU

China ipo katika mkakati wa ujenzi wa jengo refu kuliko yote duniani litakaloitwa ''Phoenix tower''. Jengo hilo linatarajiwa kumalizika kati ya mwaka 2017/2018 kuanzia ujenzi wake. jengo hilo litakalojengwa katika jimbo la  Hubei katikati mwa china linatarajiwa kuwa la kuvutia lenye rangi ya pink na litakuwa rafiki wa mazingira. Inategemewa jengo hilo litazidi jengo refu liliopo sasa la Buruj Khalifa kwa mita 172.
''Kutakuwa na mtaa wa Kifaransa, mtaa wa Kijapani, na hata mtaa wa Kituruki na mitaa mingine mingi zaidi amdayo itaruhusu watu kuiona dunia bila ya kuondoka China'' alisema Chetwood kuiambia ''The Guardian''. Mpaka sasa kuna ujenzi wa majengo mengi marefu yanayoshindana duniani ikiwemo Buruj Khalifa liliopo Dubai, na jingine ambalo ujenzi wake unategemewa kukamilika mwaka 2019 nchini Saudi Arabia litakaloitwa ''Kingdom tower'' na hili la nchini China.

Chanzo: CNN

 Hili ndo jengo refu kwa sasa la Buruj Khalifa huko Dubai


Hili ni jengo litakalo jengwa nchini Saudi Arabia litakaloitwa Kingdom Tower.





ISIS WATANGAZA UTAWALA WA KI-ISLAMU (KHILAFA)

Wapiganaji wa kiislamu wa Syria na Iraq watangaza dola ya kiislamu yaani Khilafa ikimaanisha mrejesho wa utawala huo uliomalizika takribani miaka 100 iliyopita baada ya kuanguka kwa utawala wa Ottoman. Kutokana na sauti zilizohifadhiwa na kusambazwa mtandaoni jumapili hii, utawala wa kiislamu wa Iraq  na ISIL wamethibitisha kuwa Kiongozi wao Abu Bakr Al-baghdadi kuwa ndio Khalifa wao na ndio kiongozi wa waislamu wa kila mahali. Baghdadi anaaminika kuwa kiongozi wa ISIL, ambayo ilijitangaza rasmi kuwa ni Taifa la kiislamu. Kutokana na maelezo yao, utawala huo mpya unaanzia nchini Iraq katika jimbo la Diyala mpaka Aleppo nchini Syria.
''Shura ya utawala wa kiislamu ilikutana na kujadili kuhusiana na utawala wa kiislamu. Hivyo utawala wa kiislamu uliamua kuanzisha khilafa na kumchagua khalifa wa waislamu wote'' aliarifu msemaji wa ISIL Abu Mohammad Al-Adnani.
''Majina ya 'Iraq' na 'the Levant' yameondolewa katika orodha ya taarifa muhimu ya utawala huo wa kiislamu'' alisema Adinani, akielezea kuwa utawala wa kiislam 'khilafa' ni ndoto ya waislamu wote na ni tumaini la wana-jihad wote. Inadhaniwa kuwa tangazo hilo linaweza kuleta mtafaruku kwa wapiganaji wengine wa kisunni nchini Iraq ambao wanapigana na serikali ya waziri mkuu Nour Al-Maliki na sio wanaopigana kwa ajili ya khilafa.

Chanzo: www.mwcnews.net