Assalamu Alaykum WarahmatulLahi wabarakatu.
Kwa mfano chuo cha afya Muhimbili wameelezea katika muongozo wao "prospectus" kuwa wanachagua wanafunzi watakao jiunga na Medicine/udaktari kipaumbele ni kwa waliopata alama ya B au A katika somo la Biology au Chemistry. Hii inamaanisha kwamba kama huna B au A katika masomo hayo mawili basi uwezekano wa wewe kuchaguliwa ni mdogo. Hii pia inategemea ufaulu wa wanafunzi kwani wanaweza kuchukua waliopata A pekee kama watu wengi wamefaulu au wanaweza kuchukua C kama wengi wamefeli.
Hivyo kwa maneno haya mafupi tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wote watumie vizuri muda wao kufanya uchunguzi wa vyuo na alama wanazochukua/ cutting point kabla ya kuchagua. Hii itaweza kukuweka katika nafasi nzuri ya kuchaguliwa kwani ni watu wengi ambao walipata Division One ila wakakosa vyuo kwa sababu ya kuchagua vyuo ambavyo kwa matokeo yao hawakufikia kiwango kinachohitajika.
Huu ni mfano mdogo kwa chuo cha muhimbili, hivyo kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali vyuo mbalimbali basi wanalazimika kufanya uchunguzi mdogo kama huu na kutafuta ushauri kwa wanafunzi waliomavyuoni ili wapate habari za kutosha na hatimaye kufanya uamuzi uliosahihi zaidi.