Wednesday, December 12, 2012
ABDUL JALIL AWEKEWA KIZUIZI CHA KUTOKA NJE YA NCHI
Waendesha mashtaka wa mahakama ya kijeshi nchini Libya leo wameweka marufuku ya kusafiri dhidi ya Mustafa Abdul Jalil, kiongozi wa zamani wa Baraza la Taifa la Mpito ambalo liliitawala nchi hiyo baada ya kuondolewa madarakani kwa Muammar Gaddafi. Hatua hiyo imechukuliwa ukisubiriwa uchunguzi kuhusiana na kifo cha kamanda wa waasi, Jenerali Abdel Fattah Younes, ambacho hakijapatiwa maelezo. Abdul Jalil aliongoza baraza la taifa la mpito hadi pale lilipokabidhi madaraka kwa bunge lililochaguliwa hapo Agosti mwaka huu. Anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi Februari 20 mwakani kujibu maswali yanayohusiana na kuuwawa kwa Jenerali Younes. Younes, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya Gaddafi , alijitoa kutoka serikali hiyo na kujiunga na vuguvugu la mapambano ya silaha ambalo hatimaye liliuondosha madarakani utawala wa miaka 42 wa Gaddafi mwaka jana. Younes aliuwawa Julai 2011 katika mazingira ambayo si ya kawaida baada ya kutakiwa kuondoka kutoka katika mstari wa mbele wa mapambano kwa ajili ya kuhojiwa na maafisa wa mapinduzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO