Wednesday, December 19, 2012

BAHRAIN WATUMIA HOSPITALI KUWATESA WAPINZANI

Utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain unatumia hospitali kuwatesa wapinzani. Vijana wanaharakati wa haki za binadamu huko Bahrain wameripoti kuwa utawala wa Aal Khalifa unatumia baadhi ya hospitali kuwatesea wapinzani. 

Hospitali ya Suleimaniya ni moja kati ya maeneo ambayo wapinzani hupelekwa kama majeruhi hata hivyo wakiwa huko huteswa vibaya na vikosi vya usalama vya Bahrain. Taasisi ya vijana watetezi wa haki za binadamu ya Bahrain imeashiria pia namna wapinzani wanavyowekwa na kuteswa katika hospitali hiyo na kueleza kuwa ghorofa ya kwanza na ya pili  za hospitali hiyo zimetengwa makhususi kwa ajili ya wagonjwa, lakini ghorofa za juu za hospitali hiyo hutumika kuwatia mbaroni na kuwatesa wapinzani wa utawala wa kifalme wa Aal Khalifa.  Hii ni katika hali ambayo wananchi wa Bahrain juzi walifanya maandamano makubwa huko Manama mji mkuu wa nchi hiyo na kwenye miji mingine na kutaka kung'olewa madarakani utawala wa Aal Khalifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO