Wednesday, December 19, 2012
WAMAREKANI WALAUMIANA MASHAMBULIZI UBALOZI WA BENGHAZI
Ripoti rasmi kuhusiana na mashambulizi mabaya ya mwezi Septemba dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi, imegundua kuwa kulikuwa na upungufu mkubwa katika hatua za kiusalama za wizara ya mambo ya kigeni. Katika tathmini ambayo inatoa lawama kali jopo lililopewa jukumu la uchunguzi wa tukio hilo limeelezea kuwepo kwa mapungufu kadhaa, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa watu wenye ujuzi pamoja na uongozi mbaya. Ripoti hiyo ina mapendekezo 29, ambayo yote yamekubaliwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton. Katika barua kwa kamati za bunge la Marekani, amesema kuwa ameelekeza wizara yake kutekeleza yale yaliyomo katika ripoti hiyo haraka na kwa ukamilifu wake. Maafisa wanne wa Marekani waliuawa tarehe 11 mwezi Septemba, ikiwa ni pamoja na aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya, Christopher Stevens.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO