Kundi la kisiasa la Hamas linalotawala katika Ukanda wa Gaza leo linaadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho hayo yanafanyika kwa maandamano yatakayohudhuriwa na Khaled Meshaal, kiongozi wake anayeishi uhamishoni. Meshaal aliondoka katika ardhi ya Wapalestina miaka 45 iliyopita na analiongoza kundi la Hamas kutokea Qatar na Cairo. Kiongozi huyo alishirikiana kwa karibu na serikali ya Misri, kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku nane kati ya kundi la Hamas na Israeli, yaliyotokea mwishoni mwa mwezi uliopita. Kuna uvumi kwamba ziara ya Meshaal mjini Gaza inahitimisha mchakato wa kumteua mrithi wake ambaye bado hakutangazwa hadi sasa kuliongoza kundi la Hamas.
NEXT GENERATION |
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO