Saturday, December 22, 2012

WAINGEREZA WAZIDI KUSILIMU KILA MWEZI

Kituo cha Utafiti  nchini Marekani 'Gatestone Institute' kimetoa takwimu zinazoonyesha wafuasi wa dini mbalimbali na kukiri kwamba katika kipindi cha miaka kumi ya hivi karibuni dini ya Kiislamu ndiyo iliyostawi kwa kasi zaidi nchini Uingereza na mwenendo huo utaendelea pia katika miaka ijayo. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, mamia ya Waingereza husilimu kila mwezi. Takwimu zilizotolewa na kituo hicho katika kipindi cha muongo mmoja inaonyesha kuwa, idadi ya Wakristo huko Uingereza na Wales imepungua kwa asilimia 11 ambayo ni sawa na watu milioni nne na laki moja, kwa kuporomoka kutoka watu milioni thelathini na saba na laki tatu mwaka 2001, hadi watu milioni thelathini na tatu na laki mbili mwaka 2011. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kipindi hichohicho, idadi ya Waislamu nchini Uingereza na Wales ilikua kwa asilimia 80 ambayo ni sawa na watu milioni moja na laki mbili, kutoka watu milioni moja na nusu mwaka 2001 hadi kufikia milioni mbili na laki saba mwaka 2011, huku dini ya Kiislamu ikihesabiwa kuwa ni dini ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi nchini Uingereza. Hii ni katika hali ambayo duru nyingine zinasema kuwa, idadi ya Waislamu nchini Uingereza ni kubwa zaidi kuliko hiyo iliyotangazwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO