Monday, December 17, 2012

IRAN; MKWAMO WA NYUKLIA UTATULIWE.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema nchi hiyo na mataifa makubwa lazima watafute njia ya kuondoka katika mkwamo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Ali Akbar Saleh alinukuliwa na shirika la habari la Iran ISNA, akisema pande mbili zimekubaliana kuondoka katika mkwamo wa sasa. Iran na mataifa sita - Marekani, Urusi, Ufaransa, China, Uingereza na Ujerumani wameonyesha wako tayari kuyafufua mazungumzo yenye lengo la kupata suluhu ya muafaka juu ya mgogoro wa muongo mzima kuhusiana na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo. Saleh alisema hajui ni lini duru nyingine ya mazungumzo itakapofanyika. Mataifa makubwa sita yalisema wiki iliyopita kuwa yalitarajiwa kukubaliana na Iran mapema iwezekanavyo, kufanya awamu nyingine ya majadiliano.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO