Monday, December 17, 2012

WATUNISIA NAO WAANDAMANA LEO


Wananchi wa Tunisia wameandama leo katika mji wa Sidi Bouzid kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa pili wa mapinduzi yaliyotokea nchini humo na kuung'oa madarakani utawala wa Rais Zainul Abidin bin Ali.
Waandamanaji hao waliwatupia mawe Rais Munsif al Marzouq wa Tunisia na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mustafa bin Jaafar ambaye alikuwa akijiandaa kuhutubia wananchi. Vikosi vya usalama vya Tunisia vilijibu hatua hiyo ya waandamanaji na kuwaondoa haraka viongozi hao katika eneo palipokuwa pakifanyika maandamano hayo.
Harakati za mapinduzi ya wananchi wa Tunisia ilianzia katika mji wa Sidi Bouzid baada ya mchuuzi wa biashara ndogondogo za mitaani kwa jina la Tariq Tiib Muhammad bin Bouzid kujichoma moto akilalalamikia ukandamizaji wa maafisa wa halmashauri ya mji, hatua ambayo iliibua hasira za Watunisia waliowengi na kuhitimisha utawala wa dikteta wa nchi hiyo Zainul Abidin bin Ali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO