Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi nchini Iran Meja Jenerali Hassan Firuziabadi amesema kwamba kuwekwa ngano ya kuzuia makombora nchini Uturuki kunatishia usalama na kwamba wataalamu na wenye vipaji kutoka nchi za Ulaya, Marekani na Uturuki wahakikishe mtambo huo unaondolewa kabla haujazua balaa na vita. Aidha sambamba na kuitahadharisha Uturuki kuhusu mtambo huo wa kuzuia makombora wa Jumuiya ya NATO katika ardhi yake, Meja Jenerali Firuzabadi amesema, hatua hiyo inaongeza hatari ya kuingia nchi hiyo katika vita na Syria.
Wakati huo huo Ali Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesisitiza kwamba hatua za nchi za Magharibi za kuchochea vita katika eneo ni za hatari na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitoruhusu kutekelezwa mipango na senario za nchi hizo kwa lengo la kuipindua serikali ya Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO