Sunday, December 16, 2012

KAMANDA WA VIKOSI VYA UPINZANI AUWAWA SYRIA


Jeshi la Syria limefanikiwa kumuua kamanda wa vikosi vinavyopigana dhidi ya serikali ya Damascus katika operesheni iliyofanywa na vikosi vya serikali katika mji wa kusini wa Allepo. Mkuu wa kundi la wanamgambo wa Liwal al Tawhid Yusuf al Jader aliyejulikana pia kama Abu Furat aliuawa wakati akipigana ili kudhibiti chuo cha kijeshi cha Muslimiyah kusini mwa Aleppo jana Jumamosi.
Wakati hayo yakiripotiwa, video mpya imetolewa inayoonyesha kwamba magaidi wa Syria wanaoungwa mkono na nchi za kigeni wanawapa mafunzo ya kijeshi watoto na kuwatumia katika mstari wa mbele vitani katika mapigano yao dhidi ya serikali ya Damascus. Kwa mujibu wa video hiyo magaidi wa kundi la Free Syrian Army wamewalazimisha watoto hao walio na umri wa miaka 12 kujiunga nao vitani na kuwapa mafunzo ya kupigana. Video hiyo inaonesha pia watoto hao wakilazimishwa kuchimba makaburi yao kabla ya kujiunga vitani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO