Tuesday, December 18, 2012

WACHINA WAJA NA YAO YA SIKU YA MWISHO


Serikali ya China imewatia nguvuni watu wasiopungua 93 kwa tuhuma za kueneza uvumi kuhusu kukaribia Siku ya Kiyama. Vyombo vya usalama vya China pia vimemtia nguvuni mtu mmoja aliyejeruhi watoto 23 wa shule moja baada ya kuathiriwa na tetesi za kukaribia siku ya mwisho wa dunia.
Shirika la habari la China limeripoti kuwa watu 93 wametiwa nguvuni katika mikoa saba ya nchi hiyo wakiwemo wafuasi wa kundi la kidini la "Mola Muweza" lililopigwa marufuku kwa sababu ya kusambaza matangazo yanayohubiri kwamba dunia itaangamia Ijumaa ijayo.
Shirika hilo limesema kuwa wafuasi wa kundi hilo wameamini imani zilizotangazwa na watu wanaofuata utamaduni wa Maya huko Mexico kwamba jua halitachomoza na umeme utazima tarehe 21 Disemba kwa muda wa siku tatu na hatimaye dunia itafikia mwisho.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO