Sunday, December 16, 2012

JE WEWE KATIKA HALI HIZI UNASWALI?
















Waislam wangapi leo hii wanaacha kuswali bila ya dharura za kisheria na wanaishia kudanganya. Kumbuka kuwa unajidanganya mwenyewe na jiulize nafsi yako iikiwa leo hii:
1.Umzima wa afya 
2.viungo vyote vizima huna ulemavu
3.unaishi kwenye nchi ya amani kabisa
4.unauhuru wa kufanya ibada bila ya kuulizwa na yeyote
5.hali ya hewa ni nzuri kabisa unaweza kutembea kuelekea msikitini
6.unafanya kazi ifisi nzuri na unaweza kusali hata hapoofisini kwako

Katika hali zote hizi muislam akiacha kuswali tena kwa jamaa msikitini basi ni aina moja wapo ya kuonyesha ujeuri wako tuu na si kuwa unadharura. Wafikirie waislam wa palestina wanapigwa mabomu hadi misikitini na bado wanaswali. Wewe hata risasi hujawahi kusikia lakini huswali.

Kumbuka Amali ya kwanza kabisa kuisabiwa ni SWALAAA na ikiwa imekamilika basi umashafaulu na hatoinua mja mguu wake bila ya kuhesabiwa. Jee wewe ni kundi gani?


1 comment:

TUPE MAWAZO YAKO