Watu 17 wameuawa nchini Iraq na makumi ya wenginme kujeruhiwa kufuatia matukio tofauti ya machafuko na milipuko ya mabomu katika miji mbalimbali ya nchi hjiyo. Maafisa wa polisi wanasema kuwa, milipuko miwili ya mabomu ya kutegwa garini na mingine saba iliyotokea kando kando ya barabara jirani na msikiti mmoja wa Waislamu wa madhehebu ya Ahlul Bayt AS huko Kirkuk imesababisha watu 13 kupoteza maisha yao na wengine 57 kujeruhiwa. Aidha kabla ya hapo watu wawili waliuawa baada ya bomu la kutegwa garini kulipuka katika ofisi ndogo ya Rais Jalal Talabani wa nchi hiyo katika jimbo la Diyalah. Wakati huo huo, mtu aliyekuwa na silaha amewashambulia polisi katika kituo kimoja cha upekuzi huko Tarmiyah kaskazini mwa mji mkuu Baghdad na kuwauwa wawili kati yao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO