Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, harakati hiyo katu haitautambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel na wala haiko tayari kufumbia macho hata haki ndogo kabisa ya taifa la Palestina.
Khalid Mash'al amesema hayo leo huko Gaza, Palestina katika maadhimisho ya miaka 25 ya kuasisiwa HAMAS na kusisitiza kwamba, mapambano na muqawama ndio njia pekee ya kuzikomboa ardhi zote za Wapalestina na kwamba, Hamas haitalegeza kamba katika uwanja huo. Kabla yake akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yametajwa pia kuwa ni ya kusherehekea ushindi wa Hamas dhidi ya Israel katika vita vya siku nane, Ismail Hania Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina sambamba na kusisitiza kuendelezwa muqawama dhidi ya Wazayuni amesema ushindi wa Hamas dhidi ya Israel katika vita vya siku nane ni mwanzo wa kusambaratika utawala huo ghasibu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO