Thursday, December 13, 2012

MAHAKAMA YA ICC YATAKA KESI YA GBAGBO ISIKILIZWE

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyoko The Hague nchini Uholanzi imetupilia mbali madai ya wakili mtetezi wa Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa Ivory Coast kwamba mahakama hiyo haina uhalali wa kisheria wa kusikiliza kesi hiyo. Anita Usacka Jaji wa Mahakama ya ICC amesema kuwa, awali serikali ya Ivory Coast iliitambua rasmi mahakama hiyo ya kimataifa kwani Bamba Mamadou Waziri wa zamani wa Sheria wa nchi hiyo kwa niaba ya serikali yake alitia saini hati ya kuthibitisha uhalali wa kisheria wa mahakama hiyo. Laurent Gbagbo anatuhumiwa kuhusika kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa nchini humo, baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2010 na kusababisha machafuko ya ndani. Imeelezwa kuwa watu wasiopungua 3,000 waliuawa na wengine laki tano kufanywa wakimbizi katika machafuko hayo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO