Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ameitaka Israel
aichae mpango wake wa kujenga vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika
eneo la karibu na mji wa Quds unaoukalia kwa mabavu.
Abbas amesema hayo akiwa nchini Uturuki na kuongeza kuwa, mpango huo
wa Israel wa kujenga vitongoji vipya vya walowezi karibu na mji wa Quds ni
hatari na kwamba Wapalestina hawataruhusu Tel Aviv kutekeleza mpango huo.
Wakati hayo yakiripotiwa, serikali ya Iraq imeafiki kuazishwa mfuko
wa kitaifa wa fedha kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa wa Kipalestina na Waarabu
wanaoshikiliwa katika jela za Israel. Ali al Musawi mshauri wa masuala ya habari
wa Waziri Mkuu wa Iraq Nour al Maliki amesema kwamba Baghdad imeafiki kuanzishwa
mfuko huo na itachangia dola milioni mbili.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO