Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela jana alilazwa katika hospitali mjini Pretoria kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, ingawa serikali ilisema hakukuwa na sababu ya kutaharuki. Taarifa kutoka ofisi ya rais Jacob Zuma haikuelezea kinagaubaga juu ya hali ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 94.
Mandela alilazwa hospitalini mwezi Februari kutokana na maumivu ya tumbo, lakini aliruhusiwa siku iliyofuata baada ya vipimo kuonyesha hakukuwa na jambo baya lililotokea. Mandela amekuwa kwa muda mrefu akiishi katika kijiji chake alikozaliwa cha Qunu, mashariki mwa mkoa wa Cape. Kutokana na afya yake iliyodhoofika, inamzuwia kuonekana mara kwa mara hadharani nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO