Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuipatia Eritrea uzoefu wake katika njanya mbalimbali. Ali Akbar salehi amesema hayo alipokutana na Mohamed Saeed Idris Balozi mpya wa Eritrea mjini Tehran. Aidha amesema uhusiano wa nchi mbili hizo ni mzuri na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ipo tayari kuipa Eritrea uwezo na uzoefu wake katika sekta tofauti kama biashara na uchumi.
Kwa upande wake Balozi mpya wa Eritrea mjini Tehran amekabidhi vitambulisho vya kazi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kuelezea kwamba serikali ya Asmara na wananchi wa nchi hiyo wako tayari kustawisha uhusiano na ushirikiano zaidi na Iran katika nyanja zote bila vikwazo vyovyote.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO