Marekani imefanya majaribio ya silaha hatari za nyuklia katika jimbo la Nevada ili kuhakikisha silaha zake zinaweza kutumika ipasavyo.
Majaribio hayo yametathminiwa kuwa ni ukaidi wa takwa la nchi nyingi duniani ambazo zinataka silaha za nyuklia ziangamizwe. Wizara ya Nishati ya Marekani imetoa taarifa ikisema majaribio hayo ya Jumatano iliyopita yalilenga 'kubaini uwezo wa silaha za nyuklia za Marekani'.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Marekani, ambayo ndio nchi pekee iliyowahi kutumia silaha za nyuklia dhidi ya wanaadamu, imefanya majaribio 1,032 ya silaha za nyuklia tokea mwaka 1945. Marekani ilitumia silaha za nyuklia mwaka 1945 dhidi ya miji ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki ambapo watu zaidi ya laki mbili 20 elfu waliuawa papo hapo. Katika miongo iliyofuata maelfu ya wengine walipoteza maisha kutokana na athari za mabomu hayo haribifu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO