Wednesday, December 12, 2012

MISRI WAANZA KURA YA MAONI


Wamisri karibu laki tano waishio nje ya nchi wameanza kupiga kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.Zoezi hilo limeanza katika ofisi za kibalozi za Misri katika nchi 150 kote duniani.Wakati huo huo imeripotiwa kuwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya Misri itafanyika katika siku mbili tafauti. Tume ya Uchaguzi ya Misri imesema zoezi hilo  litafanyika ndani ya nchi Desemba 15 na Desemba 22 kutokana na uchache wa majaji wanaopaswa kusimamia zoezi hilo muhimu.


Rasimu ya katiba mpya ya Misri inaungwa mkono na Chama cha Ikhwanul Muslimin cha Rais Muhammad Mursi pamoja na watu wenye misimamo ya Kiislamu nchini humo.
Huku hayo yakiripotiwa mwanasiasa mwandamizi wa upinzani Amr Mousa amesema muungano wa vyama vya upinzani unapinga rasimu ya katiba mpya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO