Kiongozi wa ngazi za juu wa kidini wa Qum hapa nchini Ayatullah Nuri Hamedani amekosoa mienendo mibaya ya Wamagharibi yenye lengo la kuzusha fitina kati ya nchi za Kiislamu.
Ayatullah Hussein Nuri Hamedani ameyasema hayo leo na kuongeza kuwa, katika fremu ya siasa za kupenda kujitanua, Marekani na Umoja wa Ulaya kwa pamoja zinaendesha siasa za kuzusha fitina kati ya nchi za Kiislamu duniani. Amesema kwamba, mwamko wa Kiislamu umewatia maadui wahaka na hofu kubwa na amewataka Waislamu kusiamama imara dhidi ya maadui wa Uislamu sambamba na kuelewa njama hizo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO