Wednesday, December 19, 2012

MUFT ASISITIZA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

Mufti wa Syria amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa ili kuhitimisha mgogoro unaoikabili nchi hiyo. Sheikh Ahmad Badruddin Hasun Mufti wa Syria amesema kuwa njama zinazofanywa na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu dhidi ya Syria zina lengo la kutoa pigo kwa utambulisho wa kiarabu na Kiislamu na kuongeza kuwa njia pekee ya kujiondoa katika mgogoro huo ni  kufanyika mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali na wapinzani wa nchi  hiyo. Sheikh Ahmad Badruddin Hasun amewaalika wapinzani wa ndani na nje ya Syria kushiriki vilivyo katika mazungumzo ya kitaifa ya nchi  hiyo na kuwataka kuungana na wananchi na mfumo wa kiraia wa Syria ili kuilinda nchi hiyo na mustakbali wake. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO