Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais Barack Obama anaunga mkono juhudi za kurejesha sheria ya kupiga marufuku sihala kali. Msemaji wa Ikulu hiyo, Jay Carney, amesema kuwa rais anaunga mkono pendekezo la seneta wa chama cha Democratic, Dianne Feinstein, kuirudisha tena sheria hiyo, baada ya mauaji yaliyotokea mjini Newtown, Connecticut. Carney ameongeza kuwa Obama pia ataunga mkono sheria ya kufunga kile alichokieleza kuwa ni mapungufu katika mauzo ya silaha. Alikuwa akizungumzia kuhusu sheria ambazo zinaruhusu watu kununua bunduki kutoka kwa wauzaji binafsi bila ya kufanyiwa uchunguzi kuhusu maisha yao. Watoto 20 na watu wazima 6 waliuwawa Ijumaa iliyopita katika shule ya msingi ya Sandy Hook na kuanzisha upya mjadala kuhusu udhibiti wa silaha nchini Marekani. Chama chenye ushawishi mkubwa cha wamiliki wa bunduki nchini Marekani kimezungumza kwa mara ya kwanza jana, na kusema kinataka kuchangia kwa dhati katika kuzuwia mauaji mengine ya halaiki.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO